Job 20:6-11


6 aIngawa kujikweza kwake hufikia mbinguni
na kichwa chake hugusa mawingu,

7 bataangamia milele kama mavi yake mwenyewe.
Wale waliomwona watauliza, ‘Yuko wapi?’

8 cKama ndoto hutoweka, wala hapatikani tena,
amefukuziwa mbali kama maono ya usiku.

9 dJicho lililomwona halitamwona tena;
mahali pake hapatamwona tena.

10 eWatoto wake watalipa yote baba yao aliyowadhulumu maskini,
nayo mikono yake itarudisha mali yote aliyonyang’anya watu.

11 fNguvu za ujana zilizoijaza mifupa yake,
zitalala naye mavumbini.

Copyright information for SwhKC